1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaushambulia mji wa Kiev kwa droni

Josephat Charo
30 Septemba 2024

Duru ya usalama ya Ukraine imesema droni 120 zimeruka zaidi ya kilometa 600 kulilenga ghala la silaha ndani ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4lDUl
Mfumo wa ulinzi wa anga dhidi ya makombora
Mfumo wa ulinzi wa anga dhidi ya makomboraPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Urusiimefanya shambulizi la droni mapema leo katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev huku vitengo vyote vya mifumo ya ulinzi wa anga wa makombora vikiingia kazini kuyazuia mashambulizi hayo. Hayo yamesemwa na jeshi la Ukraine.

Watu walioshuhudia wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wamesikia milipuko kadhaa iliyosikika kama mifumo ya ulinzi wa makombora na wameona vitu vikilengwa angani.

Mji wa Kiev na viunga vyake na eneo zima la mashariki mwa Ukraine yamewekwa katika hali ya tahadhari ya kushambuliwa kutokea angani, huku jeshi la anga la Ukraine likitahadharisha kuhusu Urusi kulilenga aneo hili kwa mashambulizi ya droni.

Haya yanajiri siku moja baada ya Ukraine kutuma droni zaidi ya 100 nchini Urusi kulishambulia ghala kubwa la silaha, huku ikiimarisha mashambulizi yake ndani zaidi ya Urusi.

Hapo jana Denmark ilitangaza kutoa msaada wa dola milioni 194 kuisadia Ukraine kuimarisha silaha zake zilizo katika shinikizo inapokabiliana na uvamizi wa Urusi.