1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatoa hakikisho la usafirishaji wa ngano

25 Julai 2022

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov ambaye kwa sasa yupo ziarani barani Afrika, ametoa hakikisho la usambazaji wa nafaka kwa Urusi muda mfupi alipowasili mjini Cairo, Misri.

https://p.dw.com/p/4Eayt
Ägypten | Treffen Sergey Lavrov und  Präsident Abdel Fattah el-Sissi
Picha: Egyptian Presidency/AP/picture alliance

Ikumbukwe tu kamwa Misri ni kati ya mataifa yenye kuaagiza kiwangio kikubwa zaidi cha ngano duniani na kwamba mwaka uliopita taifa hilo lilinunua asilimia 80 ya ngano yote inayozalishwa Urusi na Ukraine.  Lakini uvamizi wa Februari  24 wa Ukraine ulitatiza usafirishaji na iliongeza kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa duniani, na kadhalika kuteteresha mfumo wa kifedha kwa Misri.

Kutokana na vita hivyo vinavyoendelea sasa taifa hilo, Misri limegawanyika ki mahusiano kwa pande mbili, yaani mshirika wake wa muda mrefu Urusi na mataifa washirika wake wa karibu ya Magharibi, ambayo yameiwekea vikwazo Urusi na kushinkiza taifa hilo litengwe.

Jitahda za mataifa ya Magharibi katika kuitenga Urusi.

Ägypten | Treffen Sergey Lavrov und Präsident Abdel-Fattah el-Sissi
Ujumbe wa Urusi na Rais Abdel-Fattah el-Sissi Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Kabla ya ziara hii ya sasa ya Lavrov, balozi za mataifa ya Magharibi zimeonekana zikifanya ushawishi kwa Misri na Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu, uliyojumuisha mazungumzo na Rais Abdel Fattah al-Sisi na wawakilishi wa jumuiya hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na mwenzake wa Misri, Sameh Shoukry, Lavrov amesema wamedhamiria kuhakikisha wafanyabiashara wa ngano wa Urusi wanatimiza matakwa ya usafirishaji.

Aidha katika ziara hiyo ya mwanzo ya kidiplomasia nchini Misri, ambayo pia itamfikisha Ethiopia, Uganda na Jamhuri ya Congo, yenye lengo lengo la kusaka uungwaji mkono wa vita vya Urusi nchini Ukraine, Lavrov amesema Moscow inataka kuiondoa serikali iliyoko madarakani nchini Ukraine "Watu wa Urusi na Ukraine wataendelea kuishi pamoja.

kwa uhakika tutawasaidia watu wa Ukraine katika kuondokana na utawala ambao, kimsingi unapingana na watu na unapinga historia", alisema Lavrov.

Lakini kwa suala hili la shida ya upatikanaji wa ngano Lavrov amesema wamekwisha fanya mijadala maalumu ya ushirikiano, wamekubaliana katika kuendelea kuwasiliana zaidi kwa kutumia wizara husika na kwamba hadi wakati huu wanayo majibu ya kwa nini hali iimekuwa hivyo.

Soma zaidi:Urusi yasema mashambulizi bandari ya Odessa yalilenga silaha za Marakeni

Tangu kuzuke vita, kumekuwepo na vizuizi vya usafirishaji wa mizigo vinavyofanywa na Urusi katika eneo la Bahari Nyeusi, hatua ambayo imesababisha mamilioni ya tani za ngano kukwama na hivyo kusababisha usambazaji wa bidhaa hiyo katika maeneo mengine ya ulimwengu.

Ijumaa iliyopita Urusi, Ukraine, Uturuki na Marekani zilitia saini makubaliano ya kuanzisha upya usafrishaji wa ngano  kupita usafiri wa majini, lakini shambulizi la Jumamosi la  Urusi dhidi eneo la bandari la Odesa limeufanya utekelezaji wa makubaliano hayo kuwa katika hali ya mashaka.

Chanzo: RTR/AP