1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yataka UN kuingilia mazungumzo ya nafaka

20 Julai 2022

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuingilia kati mazungumzo juu ya usafirishaji wa nafaka kati ya Urusi na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4EPtk
Russland Moskau | Wladimir Putin während Videokonferenz
Picha: Mikhail Klimentyev/AP/picture alliance

Lavrov amesema Urusi ilikubali kile alichokiita "kanuni za kimsingi" kuhusu usafirishaji wa nafaka na Ukraine, lakini ujumbe wa Ukraine umekataa kujumuisha kifungu cha kulinda mauzo ya nje ya Urusi.

Ukraine na Urusi zimefanya mazungumzo chini ya upatanishi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa ili kuruhusu usafirishaji wa nafaka katika soko la kimataifa, wakati meli za kutoka bandari za Ukraine zikizuiwa kutokana na mashambulizi ya jeshi la Urusi.

Kauli ya Lavrov ameitoa siku moja tu baada ya rais Vladimir Putin kusema wakati wa ziara yake nchini Iran kuwa, mataifa ya Magharibi yanapaswa kuiondolea Urusi vikwazo vya uuzaji wa nafaka zake.

Vita vya nchini Ukraine vimeathiri pakubwa usafirishaji wa ngano na nafaka nyengine duniani na kuzua hofu ya kutokea uhaba wa chakula.