1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yashambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine

27 Agosti 2024

Watu wasiopungua saba wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya makombora na droni yaliyofanywa na Urusi katika zaidi ya nusu ya maeneo ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4jwlB
Ukraine Kramatorsk | Zerstörung nach russischem Angriff auf Hotel
Timu ya uokoaji inaendelea ya Ukraine imewasili katika hoteli iliyoharibiwa na shambulio la Urusi katika mji wa Kramatorsk, eneo la Donetsk.Picha: Genya Savilov/AFP/Getty Images

Mkuu wa jeshi la anga la Ukraine amesema Urusi imefanya moja ya mashambulizi yake makubwa zaidi ya anga dhidi ya Ukraine tangu kuzuka kwa vita hivyo.

Miundombinu ya nishati imelengwa na kusababisha kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Soma pia: Urusi yafanya mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine. 

Ukraine yote imewekwa katika hali ya tahadhari ya kutokea mashambulizi ya anga huku raia wakihimizwa kutafuta hifadhi.

Urusi imethibitisha kufanya mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine – moja ya mbinu zake za muda mrefu.