1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yashambulia bandari za Ukraine

19 Julai 2023

Urusi na Ukraine zinaripotiwa kutoa taarifa tofauti kabisa kuhusiana na mapigano yanayoendelea kaskazini mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4U6bA
Wafanyakazi wapakia nafaka Jumatano Aprili 26, 2023 katika bandari ya Izmail nchini Ukraine
Bandari ya nafaka ya Izmail nchini UkrainePicha: Andrew Kravchenko/AP/picture alliance

Haya yanafanyika wakati ambapo Urusi imeshambulia bandari za Ukraine, siku moja baada ya kujiondoa kutoka kwenye mkataba wa usafirishaji salama wa nafaka katika Bahari Nyeusi, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Urusi yasema shambulizi lake ni la kulipiza kisasi

Urusi inasema imeshambulia hifadhi za mafuta mjini Odesa na kiwanda kimoja kinachotengeneza ndege zisizokuwa na rubani, kama sehemu yake ya "mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi" kwa shambulizi la Ukraine lililoliharibu daraja la kuelekea Crimea, eneo lililo chini ya utawala wake.

UN yatafakari njia za kusafirisha nafaka za Ukraine na Urusi

Hayo yakiarifiwa, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema kwa sasa wanatafakari njia kadhaa za kusaidia kupeleka katika masoko ya kimataifa, nafaka za Ukraine na Urusi pamoja na mbolea.