1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema Ukraine imekishambulia kituo cha Zaporizhzhia

14 Machi 2024

Usimamizi wa kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya cha Zaporizhzhia kinachodhibitiwa na Urusi huko Ukraine, umesema kwamba jeshi la Ukraine limeshambulia miundo mbinu muhimu katika kinu hicho.

https://p.dw.com/p/4dVQz
Ukraine Russische Besetzung AKW Enerhodar
Mwanajeshi wa Urusi akionekana karibu na Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia Mashariki mwa UkrainePicha: Andrey Borodulin/AFP

Usimamizi wa kinu hicho unasema kifaa cha mripuko kiliangushwa karibu na uzio wa kinu hicho katika sehemu iliyo na mapipa ya dizeli.

Haijabainika wazi muda kamili ambapo shambulizi hilo lilifanyika kwani shirika la habari la reuters halikuweza kuthibitisha kwa wakati ripoti za uwanja wa mapambano kutoka pande zote mbili.

Ukraine: Usalama katika kinu cha Zaporizhzhia inazidi kuwa mbaya

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA Rafael Grossi anaripotiwa kutoa tahadhari kuhusiana na hatari inayoweza kutokea kutokana na kushambuliwa kwa kituo hicho.