Urusi yaharibu boti la Ukraine katika jaribio la shambulizi
2 Septemba 2023Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, wizara hiyo imesema kuwa hapo jana, jaribio lilifanywa na serikali ya Kyiv la shambulizi la kigaidi kwa kutumia boti iliyopakiwa nusu na isiyokuwa na rubani.
Soma pia:Mashambulizi nchini Urusi yaharibu dhana ya 'jeshi la Putin'
Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, wizara hiyo imesema kuwa hapo jana, serikali ya Kyiv ilifanya jaribio la shambulizi la kigaidi kwa kutumia boti iliyopakiwa nusu na isiyokuwa na rubani. Inasemekana kuwa boti hilo liligunduliwa na kuharibiwa kwa wakati katika Pwani ya Bahari Nyeusi.
Ukraine yasema uharibifu wa miundo mbinu ya Urusi ni faida kwake katika vita
Hakukuwa na tamko la haraka kutoka kwa maafisa wa Ukraine ambao kwa kawaida husema machache ama kukaa kimya kuhusu mashambulizi dhidi ya Urusi.