1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yasema imedungua droni za Ukraine kwenye mikoa mitano

27 Novemba 2023

Urusi imesema imezidungua ndege kadhaa zisizo na rubani zilizorushwa na Ukraine zikiilenga mikoa mitano Urusi ikiwemo mji mkuu, Moscow, ikiwa ni siku moja tangu Urusi ilipofanya shambulizi kubwa la droni mjini Kyiv.

https://p.dw.com/p/4ZTHy
Mlipuko wa droni mjini Kyiv
Mashambulizi ya kutumia droni yamekuwa yakiongezeka kila uchao kwenye mzozo kati ya Urusi na Ukraine Picha: Evgeniy Maloletka/AP PHoto/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema mifumo yake ya ulinzi imeziangusha droni 9 katika mikoa ya Tula, Kaluga, Bryansk, Smolensk na eneo la jimbo linalojumuisha mji mkuu, Moscow.

Mashambulizi hayo yanafuatia yale ya Urusi mjini Kyivambayo mamlaka za Ukraine zimesema yalihusisha ndege 75 zisizo na rubani.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita pande hizo mbili zimekuwa zikishambuliana kwa kutumia droni katika wakati mapambano makali yanaendelea kwenye uwanja wa vita.

Hivi sasa vikosi vya Urusi vinapambana kuchukua udhibiti wa mji wa viwanda wa Avdiivka, mafanikio yatakayokuwa pigo kubwa kwa Ukraine.