1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Ujerumani inajaribu kufuta historia yake ya Unazi

1 Desemba 2022

Urusi imesema leo kuwa kitendo cha Bunge la Ujerumani cha kuchukua uamuzi jana wa kuitambua njaa ya Holodomor iliyoikumba Ukraine miaka 1932-1933 kama mauaji ya halaiki yaliyoendeshwa na Utawala wa Kisovieti.

https://p.dw.com/p/4KL8f
Ukraine | Holodomor Denkmal in Kiew
Picha: Bryan Smith/ZUMA Press/picture alliance

Urusi imesema leo kuwa kitendo cha Bunge la Ujerumani cha kuchukua uamuzi jana wa kuitambua njaa ya Holodomor iliyoikumba Ukraine miaka 1932-1933 kama mauaji ya halaiki yaliyoendeshwa na Utawala wa Kisovieti, ni uchochezi dhidi yake na jaribio la Ujerumani kufuta historia yake ya Unazi.

Mnamo Novemba mwaka 1932, kiongozi wa muungano wa Soviet wakati huo Josef Stalin chini ya sheria ya kujumuisha mali kwa serikali, aliwatuma polisi kuwapokonya raia wa Ukraine nafaka, mifugo, mashamba na hata mbegu za mazao.

Mamilioni ya wakulima wa Ukraine walikufa kwa njaa katika miezi iliyofuata kwa kile wanahistoria wanasema ni "mauaji ya watu wengi na yakudhamiria".

Urusi imekataa madai kwamba hayo yalikuwa mauaji ya halaiki na kusema mamilioni ya watu katika maeneo mengine ya uliyokuwa Umoja wa KiSoviet ikiwa ni pamoja na Urusi pia waliteseka na hatua hiyo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameisifu hatua ya bunge la Ujerumani.