1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yakisahambulia kwa droni kituo cha nishati cha Sumy

6 Julai 2024

Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika kituo cha nishati katika mkoa ya Sumy kaskazini mashariki mwa Ukraine usiku wa kuamkia leo. Hayo yamesemwa na maafisa wa eneo hilo

https://p.dw.com/p/4hxj4
Ukraine
Urusi imeendeleza mashambulizi yake ya droni nchini Ukraine. Mara hii imekishambulia kituo cha nishati katika mkoa wa SumyPicha: DW

Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika kituo cha nishati katika mkoa ya Sumy kaskazini mashariki mwa Ukraine usiku wa kuamkia leo. Hayo yamesemwa na maafisa wa eneo hilo.Jeshi la anga la Ukraine limesema kuwa wadunguaji wake wa droni walizinasa droni 24 kati ya 27 zilizorushwa na Urusi kwenye mikoa 12.

Soma zaidi.Hamas yakubali pendekezo la Marekani juu ya mateka wa Israel 

Kampuni inayosimamia shughuli za gridi ya taifa Ukrenergo ilisema kuwa kituo chake cha nishati katika eneo la Sumy kimeharibiwa na kupelekea kukatika kwa umeme kwa watumiaji wa viwandani na mpaka sasa bado timu ya maafisa wanaofanya matengenezo inapampabana kuurejesha umeme.

Tangu mwezi Machi, vikosi vya Urusi vimeongeza mashambulizi ya nguvu katika maeneo ya nishati ya Ukraine na kusababisha kukatika kwa umeme na kupungua kwa uzalishaji wa mafuta na maji kwa muda mrefu.