1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yakataa azma ya Ujerumani kupata kiti cha kudumu UN

3 Januari 2025

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya, katika mahojiano yaliyorushwa na televisheni ya taifa ya Urusi amesema nchi yake itapinga Ujerumani kupata kiti cha kudumu kwenye Umoja huo.

https://p.dw.com/p/4onhM
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vasily NebenzyaPicha: Spencer Platt/Getty Images

Nebenzya amesema iwapo baraza hilo lingefanyiwa mageuzi, baadhi ya nchi kamwe haziwezi kuwa wanachama wa kudumu, hata ikiwa zingetamani kufanya hivyo.

Amesema anazungumzia hasa kuhusu Ujerumani na Japan. Madajiliano kuhusu mageuzi katika Baraza la Usalama yamekuwa yakiendelea kwa miaka mingi ndani ya Umoja wa Mataifa.

India na nchi za Afrika zina matumaini ya kupata kiti cha kudumu katika baraza hilo. Hata hivyo, kwa muda mrefu serikali ya Ujerumani nayo imekuwa na azma hiyo.