1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yakabiliwa na vikwazo

22 Februari 2022

Bunge la Urusi limepitisha agizo la Rais Vladimir Putin la kutambua uhuru wa maeneo ya waasi mashariki mwa Ukraine, siku moja baada ya Rais Putin kutia saini agizo hilo na kuamuru wanajeshi kuingia katika maeneo hayo.

https://p.dw.com/p/47QmP
Russland Präsident Putin TV-Ansprache an Nation
Picha: Alexey Nikolsky/Kremlin/SPUTNIK/REUTERS

Huku haya yakijiri Urusi inakodolea macho vikwazo kutoka nchi za magharibi kuhusiana na mgogoro unaoendelea kufukuta kati yake na Ukraine. somaUrusi yatambua rasmi uhuru wa majimbo ya Ukraine 

Agizo hilo limeungwa mkono kwa kauli moja katika baraza la wawakilishi mjini Moscow. Mabalozi wa Urusi katika mataifa kadhaa ya Ulaya, yakiwemo Austria na Uingereza, wametakiwa kufika katika wizara za mambo ya kigeni za mataifa hayo kujieleza kuhusiana na agizo la jana la Rais Vladimir Putin.

Taarifa kutoka kwa wakuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, na Charles Michel imesema umoja huo unatafakari kuwekea vikwazo benki za Urusi zilizo na matawi katika maeneo ya majimbo yanayodhibitiwa na waasi wa Ukraine ya Luhansk na Donetsk. Hata hivyo vikwazo hivyo vitahitaji ridhaa kutoka kwa nchi zote 27 wanachama.

somaUrusi yawakosoa viongozi wa Magharibi kutabiri vita na Ukraine

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Uingereza itaweka vikwazo kwa benki tano za Urusi na watu watatu "wenye hadhi ya juu" kufuatia kutumwa kwa wanajeshi katika mikoa miwili inayoungwa mkono na Moscow.

Bomba la gesi kusitishwa

Brüssel von der Leyen und Kanzler Scholz
Kansela wa UJerumani na mkuu wa Umoja Ulaya Ursula von der LeyenPicha: JOHANNA GERON/AFP/Getty Images

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametangaza kuwa mchakato wa kuidhinisha matumizi ya bomba la gesi la Nord Stream 2 umesimamishwa. Ujenzi wa bomba hilo linaloziunganisha Ujerumani na Urusi kupitia chini ya bahari umekamilika, lakini utata unaolizunguka umelizuia kuanza kufanya kazi hadi sasa.

Aidha kansela Scholz amesema "Rais wa Ukraine Zelenskiy anastahili heshima yetu kubwa, kwamba nchi yake haikubali kuchokozwa na Urusi, kwa sababu ndicho hasa Rais wa Urusi anachosubiri, ili kuwa na kisingizio cha kuteka Ukraine nzima."

NATO kufanya mazumgumzo na Ukraine

Deutschland NATO-Generalsekretär Jens Stoltenberg
Mkuu wa NATO Jens StoltenbergPicha: Tobias Hase/dpa/picture alliance

 

Jumuiya ya kujihami yaNATOnayo imetangaza kufanya mkutano "usio wa kawaida" leo Jumanne na mjumbe wa Ukraine baada ya Urusi kutambua kanda mbili zinazojitenga mashariki mwa nchi hiyo.

Muungano huo umesema mkuu wa NATO Jens Stoltenberg atatoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya mazungumzo na Ukraine ambaye si mwanachama wa NATO.

Ujerumani nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya kupitia waziri wake wa Ulinzi Christine Lambrecht imesema iko tayari kupeleka wanajeshi zaidi katika jimbo la Baltiki la Lithuania, huku kukiwa na ongezeko la hofu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Hata hivyo naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Andrey Rudenko amepuuza mfululizo wa vikwazo vya nchi za magharibi dhidi ya nchi yake akisema Urusi haiogopi chochote.

 

AFP/dpa