1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaiashambulia vikali Ukraine usiku wa kuamkia Ijumaa

10 Februari 2023

Vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi makali katika maeneo tofauti ya Ukraine usiku wa kuamkia Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4NK1h
Ukraine Region Saporischschja | Zerstörung
Picha: Dmytro Smolienko/Photoshot/picture alliance

Katika hatua za mapema takribani makombora 17 yamevurumishiwa katika mji wa kusini/mashariki wa taifa hilo wa Zaporizhzhia.

Gavana wa eneo la kusini mwa Ukraine la Udesa, Maksym Marchenko amesema kumekuwa na mashambulizi ya anga na meli za kivita zilizobeba makombora katika eneo la bahari.

Mashambulizi yamesababisha kelele za ving'ora vya tahadhari hadi asubuhi ya leo hatua ambayo imesababisha maafisa kuwataka raia kujihifadhi kwa hofu ya kutokea mashambulizi mengine zaidi.

Miundombinu muhimu pia imeshambuliwa katika mji wa Khmelnitskyi magharibi Ukraine, Kharkiv kaskazini mashariki na mkoa wa Dnipropetrovsk katikati mwa Ukraine.