1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yashambulia maeneo kadhaa ya Ukraine usiku kucha

19 Julai 2023

Urusi ilifanya mfululizo wa mashambilizi makali ya angani usiku kucha kwa kutuma droni na kufyatua makombora kuelekea maeneo ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4U795
Shambulizi la kombora la Urusi katika eneo la Odessa mnamo Juni 14,2023
Shambulizi la kombora la Urusi katika eneo la OdessaPicha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Mashambulizi hayo yaliulenga mji wa bandari wa kusini wa Odesa kwa usiku wa pili mfululizo, na kuwajeruhi karibu watu 12. Wakati huo huo, maafisa wa huduma za dharura wa Urusi katika rasi ya Crimea wamesema zaidi ya watu 2,000 walihamishwa kutoka vijiji vinne kwa sababu ya moto uliotokea kwenye kituo cha kijeshi. Moto huo pia ulisababisha kufungwa kwa barabara moja kuu muhimu.

Urusi yataja mashambulizi hayo kuwa ya kulipiza kisasi

Mashambulizi hayo ya karibuni yamejiri siku moja baada ya Urusi kufanya kile Wizara ya ulinzi ya Moscow ilikielezea kuwa "shambulizi la kulipiza kisasi katika vituo vya kijeshi vya Ukraine karibu na Odesa na mji wa pwani wa Mykolaivm kwa kutumia zana zilizofyatuliwa kutokea baharini.