1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafanya mashambulizi makubwa ya makombora mjini Kiev

16 Mei 2023

Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya makombora katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv ambapo milipuko imeendelea kusikika hadi mapema leo asubuhi. Moscow ilirusha msururu wa makombora kutoka angani, baharini na nchi kavu.

https://p.dw.com/p/4RPOc
Ukraine Bachmut | Soldat der Wagner Gruppe
Picha: Valentin Sprinchak/TASS/IMAGO

Serhii Popko, mkuu wa shughuli za kijeshi mjini Kyiv amesema mashambulizi hayo ni ya nadra kutokana na idadi kubwa ya makombora yaliyorushwa ndani ya muda mfupi. Hata hivyo Popko amebaini kuwa idadi kubwa ya makombora hayo yaliharibiwa na mfumo wa ulinzi wa anga.

Zelenskiy azuru Uingereza, apata ahadi ya silaha zaidi

Hii ni mara ya nane ndani ya mwezi huu kwa mashambulizi ya anga ya Urusi kuulenga mji wa Kyiv, hii ikidhihirisha wazi kuongezeka kwa hali ya mvutano baada ya wiki kadhaa za utulivu na kabla ya mashambulizi ya Ukraine yanayotarajiwa hivi karibuni.