1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yaishambulia mikoa ya Kherson na Kharkiv

8 Januari 2024

Watu wawili wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Kherson, kufuatia shambulio la makombora la Urusi.

https://p.dw.com/p/4axW6
Ukraine Cherson | Zerstörungen nach Angriffen | Ukrainische Su-25
Ndege za kivita za Ukraine huko Kherson: 28.12.2024Picha: Oleksandr Ratushniak/REUTERS

Gavana wa kijeshi wa mkoa huo Oleksandr Prokudin, ametoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram.

Prokudin amesema Urusi imeushambulia mji huo uliopo kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi kwa makombora na droni huku maeneo kama soko na majengo kadhaa ya makazi yakilengwa. Gavana wa mkoa wa Kharkiv Oleh Syniehubov ametoa taarifa ya eneo lake pia kulengwa na mashambulizi.

Soma pia: Ukraine: Urusi ilitumia makombora iliyopewa na Korea Kaskazini.

Kharkiv na mji mwingine ulioshambuliwa wa Vovchansk ziko karibu na mji wa mpakani wa Belgorod wa Urusi ambao ulishambuliwa vikali na Ukraine hivi majuzi na kupelekea Moscow kuahidi kulipiza kisasi. Urusi imekuwa ikiendesha vita vyake vya uvamnizi nchini Ukraine kwa karibu miaka miwili sasa.