1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yaendeleza mashambulizi mashariki ya Ukraine

2 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameelezea mashambulizi ya kutisha yanayofanywa na vikosi vya Urusi ambavyo vinasonga mbele kuelekea kwenye jimbo la Donetsk.

https://p.dw.com/p/4N0Pd
Ukraine Krieg | Kramatorsk
Picha: Yevgen Honcharenko/AP/dpa/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameelezea mashambulizi ya kutisha yanayofanywa na vikosi vya Urusiambavyo vinasonga mbele kuelekea kwenye jimbo la Donetsk.

Zelensky amesema hali imekuwa ngumu zaidi kuelekea eneo la mashariki mwa Ukraine. Amesema mji wa Bakhmut na jamii nyingine 10 zilishambuliwa jana kwa makombora na vifaru vya Urusi. Aidha, Naibu Waziri wa Ulinzi, Hanna Malyar amesema mashambulizi makali yamefanyika katika mji muhimu wa kimkakati wa Lyman.

Amesema miji ya Avdiivka na Maryinka pia ililengwa. Wakati huo huo, Gavana wa jimbo la Donetsk Pavlo Kyrylenko amesema watu wapatao wawili wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa katika shambulizi la roketi la Urusi lililotokea kwenye mji wa Kramatorsk.