Urusi yadungua droni tisa za Ukraine karibu na Moscow
14 Desemba 2023Matangazo
Shambulizi hilo lililoripotiwa, lilitokea saa chache kabla ya rais wa nchi hiyo Vladmir Putin kufanya mkutano wake wa kwanza na wa mwisho wa mwaka na wanahabari tangu kuanzisha mashambulizi nchini Ukraine mwezi Februari 2022, na siku moja baada ya shambulio la kombora la Urusi kujeruhi mamia ya watu mjini Kyiv.
Soma pia:Urusi yarusha makombora, droni 23 kuelekea Ukraine
Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Urusi, imesema kuwa vitengo vya ulinzi wa anga vilivyokuwa vikishika doria viliharibu na kunasa ndege hizo tisa zisizo na rubani katika maeneo ya Kaluga na Moscow na kuilamu Ukraine kwa shambulizi hilo.
Meya wa Moscow Sergei Sobyanin amesema ndege moja ililengwa na kuangushwa karibu na Naro-Fominsk, mji ulioko Kusini Magharibi mwa Moscow.