1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine na Urusi zadai kuzima mashambulizi ya droni

3 Novemba 2023

Serikali ya Ukraine imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga imedungua usiku wa kuamkia Ijumaa, dazeni mbili za ndege zisizo na rubani za Urusi na kombora.

https://p.dw.com/p/4YM49
Picha hii iliyopigwa Julai 31, 2023, yaonesha makombora yaliyofyatuliwa na Urusi kutoka eneo la Belgorod la Urusi yakikiwa angani kuelekea upande wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine.
Picha hii iliyopigwa Julai 31, 2023, yaonesha makombora yaliyofyatuliwa na Urusi kutoka eneo la Belgorod la Urusi yakikiwa angani kuelekea upande wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine.Picha: Vadym Bielikov/AFP

Mashambulizi hayo yalilenga mji wa pili kwa ukumbwa nchini Ukraine wa Kharkiv. Gavana wa mkoa huo Oleh Synehubov amesema mashambulizi hayo yalilenga miundombinu ya kiraia, wakati kukiwa na wasiwasi juu ya kuongezeka kwa mashambulio dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine wakati wa msimu huu wa baridi.

Kwa upande wake Urusi imetoa taarifa ambayo haikuweza kuthibitishwa kuwa imedungua pia droni 29 za Ukraine karibu na kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya cha Zaporizhzhya na kuzima mashambulio matano katika rasi ya Crimea.