1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yadai kukamata maeneo zaidi ya Bakhmut

23 Aprili 2023

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema hii leo kwamba majeshi yake yameyakamata maeneo zaidi ya mji wa Bakhmut nchini Ukraine, wakati wakiendeleza jaribio la kutwaa udhibiti kamili wa jiji hilo.

https://p.dw.com/p/4QSUl
Mkaazi wa jiji la Bakhmut nchini Ukraine akipita mbele ya majengo yaliyoharibiwa vibaya na mashambulizi ya kulidhibiti eneo hilo.
Mashambulizi makali zaidi yameshuhudiwa hivi karibuni katika jiji la Bakhmut na kusababisha uharibifu mkubwa. Picha: KAI PFAFFENBACH/REUTERS

Wizara hiyo imesema vikosi vyake vimeyakamata maeneo mawili zaidi katika wilaya za magharibi za Bakhmut na vikosi vyake vya anga vimekuwa vikiendeleza mashambulizi katika maeneo ya kaskazini na kusini.

Kumeshuhudiwa vita vikali vya kugombea eneo hilo lililoharibiwa vibaya na mashambulizi ya makombora.

Urusi imesema udhibiti wa Bakhmut, utawarahisishia kufanya mashambulizi zaidi mashariki mwa Ukraine na uwezekano wa vikosi vyake kukabiliwa na mashambulizi makali zaidi katika miji mikubwa ianyopakana na Bakhmut ya Kramatorsk and Sloviansk.