1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi, Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha

9 Februari 2024

Urusi na Ukraine zimerushiana jumla ya droni 35 usiku kucha, majeshi ya nchi hizo mbili yamesema leo Ijumaa, huku pande zote mbili zikifanya majaribio ya usiku kucha kuvunja mkwamo katika vita baina yao.

https://p.dw.com/p/4cDMy
Madhara ya mashambulizi ya jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Madhara ya mashambulizi ya jeshi la Urusi nchini Ukraine.Picha: Valentin Sprinchak/Tass/IMAGO

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema jeshi lake lilidungua froni 19 za Ukraine katika mikoa minne tofauti na Bahari Nyeusi, huku Ukraine ikisema iliangusha droni 10 kati ya 16 zilizorushwa na Urusi.

Soma zaidi: 

Katika miezi yaUrusi, Ukraine zabadilishana mamia ya wafungwa karibuni Ukraine imeongeza mashambulizi yake ya droni dhidi ya Urusi, yakilenga hasa mikoa ya mpakani, lakini pia mji mkuu Moscow, na mji wa kaskazini wa Saint Petersburg.

Soma zaidi: Urusi yaivurumishia mvua ya makombora Ukraine

Imeshambulia vituo kadhaa vya nishati, katika kile ambacho Kyiv, imekiita kisasi cha "haki" kwa mashambulizi ya Moscow yanayolenga vituo vya umeme kote nchini Ukraine.