1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi, Ukraine zaendelea kushambuliana

4 Agosti 2024

Urusi imesema leo kuwa, wanajeshi wake wamefanikiwa kukidhibiti kijiji cha Novoselivka Persha mashariki mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4j5tw
Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine
Vita vya Ukraine vinaendelea huko katia kijiji Novoselivka Persha, Avdiivka, Ukraine Februari 20, 2024.Picha: Narciso Contreras/Anadolu/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vilikikomboa kijiji hicho kinachopatikana katika eneo la Donetsk ambako vikosi vyake vimekuwa vikifanya mashambulizi.

Katika hatua nyingine, ndege moja isiyo na rubani ya Ukraine imemuuwa mwanamke mmoja katika mji wa Shebekino kwenye eneo la Belgorod nchini Urusi. Taarifa hiyo imethibitishwa Gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov leo Jumapili.  Wakati huohuo, maafisa wa Moscow wamesema, Ukraine imeishambulia na kuizamisha manowari ya kivita ya Urusi.

Kulingana na maafisa hao, droni moja ya Ukraine ilishambulia pia jengo lililokuwa na mfumo wa anga kuzuia makombora. Mfumo huo ulikuwa ukitumika kulilinda daraja la Kerch ambalo ni muhimu kwa kusafirishia  na kusambaza vifaa muhimu kwa vikosi vya Urusi.