1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVietnam

Urusi na Vietnam zaazimia kuimarisha uhusiano

20 Juni 2024

Urusi na Vietnam zimeahidi kuimarisha uhusiano, wakati ambapo Rais Vladimir Putin anafanya ziara ya kiserikali nchini humo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.

https://p.dw.com/p/4hJsC
Rais Putin ziarani Hanoi
Urusi na Vietnam zimeazimia kuimarisha ushirikiano katika wakati Urusi inakabiliwa na vikwazoPicha: Minh Hoang/AP Photo/picture alliance

Urusi na Vietnam zimesema katika taarifa ya pamoja kwamba ushirikiano wao wa kiulinzi na usalama hauelekezwi dhidi ya nchi yoyote bali unachangia katika kudumisha amani, utulivu na maendeleo endelevu.

Marais To Lam na Vladmir Putin wametia saini mikataba ipatayo kumi na mbili ya ushirikiano juu ya elimu, haki na miradi ya nyuklia kwa matumizi ya amani.

Putin aliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yake yalikuwa ya manufaa na kwamba Urusi na Vietnam zina misimamo sawa na inayokaribiana katika masuala muhimu ya kimataifa.