1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita

4 Februari 2023

Wafungwa kadhaa wa kivita wa Urusi na Ukraine wamerejea nyumbani kufuatia mpango wa kubadilishana wafungwa. Mshauri mwandamizi katika ofisi ya rais Andriy Yermak amesmea kuwa wanajeshi 116 wa Ukraine wameachiliwa huru

https://p.dw.com/p/4N6W0
Gefangenenaustausch zwischen Russland und Ukraine
Picha: UKRAINIAN ARMED FORCES/REUTERS

 Amesema wafungwa wa kivita walioachiwa wanajumuisha waliokuwa katika mji wa Mariupol wakati wa mzingiro wa miezi kadhaa wa Moscow, pamoja na wapiganaji kutoka mkoa wa Kherson na walenga shabaha waliokamatwa wakati wa mapambano makali yanayoendelea ya kuudhibiti mji wa mashariki wa Bakhmut.

Maafisa wa Ulinzi wa Urusi nao wametangaza kuwa askari 63 wa Urusi wamerejea nyumbani kutoka Ukraine kufuatia ubadilishanaji huo wa wafungwa, wakiwemo wafungwa wa kile kilichotajwa kuwa "kitengo maalum" ambao kuwachiwa kwao kulitokana na mazungumzo ya upatanishi na Umoja wa Falme za Kiarabu.