Urusi, Ukraine wabadilishana wafungwa wa kivita zaidi ya 200
11 Aprili 2023Makubaliano hayo yamefanikisha kiasi cha wanajeshi 200 waliokuwa wakishikiliwa katika pande zote za mzozo kurejeshwa kwenye mataifa yao.
Rais Zelensky amesema mpango huo umefanikisha wanaume 80 na wanawake 20 kurejea Ukraine na miongoni mwao ni pamoja na waliopambania jiji la Mariupol na kiwanda cha chuma cha Azovstal, ambacho kipo chini ya udhibiti wa Moscow tangu miezi ya mwanzo ya vita.
Soma pia: Urusi, Ukraine zabadilishana wafungwa
Wizara ya Ulinzi Moscow imesema askari wake waliokuwa wakishikiliwa na Kyiv wameachiliwa baada ya mchakato wa mazungumzo. Urusi na Ukraine mara kadhaa zimekuwa zikibadilishana wafungwa wa kivita tangu mwanzoni mwa uvamizi wa Moscow mnamo Februari 2022, ikiwa ni mfano wa nadra wa mawasiliano ya bayana baina ya mahasimu.