1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kutozivamia Poland, Latvia

9 Februari 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema hana mpango wa kuivamia Poland, Latvia ama eneo jingine lolote na wala hana nia ya kuvipanua vita vyake nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cD7E
Vita vya Ukraine - Mahojiano ya Putin na Carlson
Rais Vladimir Putin wa Urusi kwenye mahojiano yake na mwandishi wa televisheni wa Marekani, Tucker Carlson.Picha: Tucker Carlson Network/REUTERS

Putin amesema hayo kwenye mahojiano na mtangazaji wa televisheni wa nchini Marekani Tucker Carlson yaliiyorekodiwa siku ya Jumanne mjini Moscow.

Soma zaidi: Urusi na Ukraine zashambuliana usiku wa kuamkia leo

Lakini Putin amesisitiza kwamba watachukua hatua ikiwa Poland itaivamia Urusi na kuongeza kuwa hana maslahi yoyote nchini humo wala Latvia na eneo jingine lolote na kwa maana hiyo hawaoni sababu ya kuwavamia.

Soma zaidi: Xi, Putin waituhumu Marekani kuingilia nchi zao

Putin aidha ameyahakikishia mataifa ya Magharibi kwamba kamwe Urusi haitashindwa katika vita vyake nchini Ukraine na kuitaka Jumuiya ya Kujihami ya NATO kukubaliana na hatua ya Urusi ya kuyanyakua maeneo nchini humo.