Urusi kulipiza kisasi jaribio la 'kumuua Putin'
5 Mei 2023Matangazo
Urusi inaishutumu Ukraine kwa kurusha ndege hiyo katika ikulu ya Kremlin katika jaribio la kumuua Rais Vladmir Putin.
Urusi imesema Marekani inahusika kupanga shambulizi hilo.
Akizungumza leo na waandishi habari nchini India, Lavrov amesema ni wazi kwamba "magaidi wa Ukraine wasingeweza kufanya hivyo peke yao bila Marekani kufahamu."
Soma zaidi: Ukraine: Putin azuru mikoa miwili inayokaliwa na Urusi
Hata hivyo, Ukraine imekanusha madai hayo na Marekani imeyapuuza ikisema ni ya "uongo".
Wakati huo huo, kiongozi wa kundi binafsi la kijeshi la Urusi, Wagner, Yevgeny Prigozhin amesema kikosi chake kitaondoka Bahkmut, Ukraine Mei 10.
Prigozhin amesema leo kuwa wataondoka kwa sababu ya kupoteza wapiganaji wake wengi na ukosefu wa silaha.