1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kujenga reli Mashariki mwa Ukraine

5 Julai 2022

Mchakato wa kuidhinisha Sweden na Finland kuwa wanachama wapya wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO umezunduliwa, hatua ambayo jumuiya hiyo inaiita ya kihistoria iliyosababishwa na vita vya Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Dfz2
NATO unterzeichnet Beitrittsprotokolle für Finnland und Schweden
Picha: Wiktor Nummelin/TT NYHETSBYR?N/picture alliance

Katika mkutano wake wa pamoja kwa waandishi wa habari na mawaziri wa mambo ya nje wa Finland na Sweden, Jens Stoltenberg amesema  hii ni siku nzuri kwa mataifa hayo. Na kuongeza kwa kusema mkutano huo unayoyakutanisha mataifa 32,  utafanikisha usalama zaidi na raia wa mataifa husika kadhalika watakuwa salama zaidi, katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na kitisho kikubwa kabisa cha kiusalama katika miongo kadhaa.

Ujenzi wa Reli ya kuunganisha Urusi na Ukraine.

Ukraine | Zerstörung in Lyssytschansk
Hali ya mkoa wa LuhanskPicha: Luhansk region military administration/AP/picture alliance

Ndani nchini Ukraine, Urusi ina mpango wa kuanzisha ujenzi wa reli amabyao inaunganisha mji wake wa kusini wa Rostov na mengine ya mashariki mwa Ukraine ya Donetsk na Luhansik. Habari hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la TASS, likinukuu serikali ya mkoa wa Rostov.

Jumapili iiliyopita Urusi iliyaweka mazingira ya udhibiti kamili wa mkoa wa Luhansk na kwa sasa ipo katika mapigano makali yenye lengo la kuwaondoa kabisa wanajeshi wa Ukraine katika viunga vya mji wa Donetsk.

Wakati mapigano yakindelea balozi wa Marekani kwa Ukraine, Bridget Brink  amezuru katika kituo kimoja cha kijeshi cha mjini Kyiv, pamoja na mambo mengine ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Uhuru wa Marekani. Zaidi anasema "Siwezi kutabiri ni lini vita hivi vya kikatili vya Urusi dhidi ya Ukraine vitaisha, lakini naweza kutabiri hili: Ukraine itashinda, na tutasimama na Ukraine kwa kadri itakavyowezekana."

Ujenzi mpya wa Ukraine ni wa muda mrefu.

Ukraine Recovery Conference | Lugano, Schweiz
wajumbe wa mkutano wa LuganoPicha: Alessandro della Valle/EDA/KEYSTONE/picture alliance

Nje ya Ukraine, katika mkutano wa kimataifa ya kuweka mpango ya ujenzi mpya wa taifa hilo huko Lugano Uswisi, Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Svenja Schulze ametahadharisha kwamba kutahitajika jitihada kubwa ya katika kuijungea mpya Ukraine. Akizungumza na shirika la habari la Ujerumani DPA, Schulze amesema mradi huo si wa mwaka mmoja au miwili.

Katika mazungumzo hayo yalianzoa Jumatatu, Waziri Mkuu wa Ukraine, Danys Shmyhal alisema ujenzi wa miuondimbinu ya Ukraine utahitaji Euro bilioni 750. Waziri Schulze anasema hatua hiyo pia itatoa fursa kwa Ujerumani kwa kusema Ukraine ni nchi kubwa. Kabla ya vita na watu wengine kulikimbia taifa hilo Ukraine ilikuwa na watu karibu milioni 44.

Vyanzo: AFP/RTR/DPA