1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi kuchunguza video ya kuchinjwa mwanajeshi wa Ukraine

13 Aprili 2023

Urusi imesema leo kuwa wanajeshi wake wanavizuia vikosi vya Ukraine kuingia na kutoka katika mji uliozongwa na mapigano wa Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4Q19z
Russland - Ukraine -Krieg I  Bakhmut
Picha: Libkos/AP/picture alliance

Ukraine bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na mapambano hayo marefu na yaliyoshuhudia umwagikaji mkubwa zaidi wa damu tangu kuanza kwa vita nchini humo.

 Ila mkuu wa kampuni ya askari wa kibinafsi ya Urusi Wagner Group, Yevgeny Prigozhin, amesema ni mapema mno kusema kwamba mji wa Bakhmut umezingirwa.

Soma pia: Zelensky ataka viongozi wa dunia kuchukua hatua haraka kufuatia video ya kuchinjwa kwa mfungwa wa kivita.

Huku hayo yakiarifiwa, afisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Urusi, imesema inafungua mashtaka ya mwanzo kuhusiana na ukanda wa video unaoonyesha kuchinjwa kwa mfungwa wa kivita wa Ukraine.

Kuibuka kwa video hiyo ambayo shirika la habari la Ufaransa AFP haikuweza kuthibitisha, kulizusha ghadhabu nchini Ukraine. Hatua hii si ya kawaida kwa Urusi ambayo kwa kawaida hukataa waziwazi madai ya uhalifu wa kivita.