1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi huenda isirefushe mpango wa usafirishaji nafaka

5 Julai 2023

Urusi imesema haioni msingi wa kurefusha mkataba wa usafirishaji nafaka katika Bahari Nyeusi, ikiwa ni chini ya wiki mbili kabla ya muda wa makubaliano hayo kumalizika.

https://p.dw.com/p/4TQrJ
Ukraine I usafirishaji nafaka
Wafanyakazi wakipakia nafaka katika bahari ya Izmail UkrainePicha: Andrew Kravchenko/AP/picture alliance

Urusi imesema haioni msingi wa kurefusha mkataba wa usafirishaji nafaka katika Bahari Nyeusi, ikiwa ni chini ya wiki mbili kabla ya muda wa makubaliano hayo kumalizika. Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi imesema meli zote zilizo chini ya mpango huo zinapaswa kuondoka katika bandari za Bahari Nyeusi kabla ya kumalizika muda wake. Muafaka huo utafikia mwisho Julai 17. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mapema wiki hii walitoa wito wa kurefushwa makubaliano hayo. Mpango huo unaruhusu nafaka na mbolea kusafirishwa kutoka bandari tatu za Ukraine katika Bahari Nyeusi. Ulifikiwa Julai mwaka jana chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na Uturuki kwa awamu ya kwanza ya siku 120. Hatua hiyo ililenga kupambana na mzozo wa chakula duniani uliozidishwa na uvamizi wa Moscow nchini Ukraine. Nchi hizo mbili ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa nafaka duniani. Mkataba huo ulirefushwa mara tatu tangu ulipotiwa saini.