1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ureno yaifunga Finland huku Italia ikikabana koo na Uturuki

5 Juni 2024

Kiungo wa Man U Bruno Fernandes aliingia kama mchezaji wa akiba na kufunga magoli 2 na kuisaidia Ureno kuanza mechi zake za kupasha misuli moto kuelekea mashindano ya Euro mwaka 2024 kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Finland.

https://p.dw.com/p/4geyK
Manchester United's Bruno Fernandes
Bruno Fernandes wa Manchester United akiwapongeza mashabiki kufuatia mechi ya raundi ya nne ya Kombe la Carabao kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester. Tarehe ya picha: Jumatano Novemba 1, 2023.Picha: picture alliance/empics

Mechi hiyo imechezwa mjini Lisbon usiku wa kuamkia leo. Mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Ruben Dias na Diogo Jota huku Teemu Pukki akiwafungia Finland ambao hawajafuzu mashindano ya Ulaya yatakayokuwa Ujerumani, mabao yote mawili. Ureno ilimkosa nahodha wao Cristiano Ronaldo ambaye yuko mapumzikoni kabla kuripoti kambini ijumaa wiki hii, akitazamia kushiriki mashindano hayo ya Ulaya kwa mara ya sita. Kutokana na hilo kocha Roberto Martinez alikibadilisha kikosi chake pakubwa ila kiliutawala mchezo kuanzia mwanzo wa mechi. Katika mechi nyengine ya kirafiki, mabingwa watetezi wa taji la Euro Italia walizuiwa sare ya kutofungana na Uturuki huko mjini Bologna.