1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Zimbabwe wataka serikali ya mpito

24 Oktoba 2018

Kiongozi wa Upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa, ameomba serikali ya mpto iundwe nchini humo haraka iwezekanavyo ili kutatua matatatizo ya kiuchumi na kisiasa.

https://p.dw.com/p/376he
Bildkombo Simbabwe Präsidentschaftswahlen Mnangagwa Chamisa
Picha: picture-alliance/AP Photo

Kiongozi  mkuu  wa  upinzani  nchini  Zimbabwe Nelson Chamisa ametoa  wito jana  wa  kuundwa  serikali  ya  mpito  kutatua  hali mbaya  ya  kiuchumi  na  mzozo  wa  kisiasa  unaoikumba  nchi  hiyo. Upungufu  wa  fedha  za  kigeni  katika  wiki  za  hivi  karibuni umezusha  mzozo  mkubwa  wa  kiuchumi ambapo  upatikanaji  wa  mafuta , chakula  na  madawa  unapungua. Hatua  ya  kwanza  ni kwa  nchi  hii  kuingia  katika  njia  ya  mjadala  wa  kisiasa, amesema  chamisa  mwenye  umri  wa  miaka  40, kiongozi  wa  chama cha Movement for Democratic Change MDC, ambaye  amedai  kwamba  ameshinda  uchaguzi  wa  rais  wa  hapo Julai 30. Chamisa ambaye  alishindwa  na  rais  wa  sasa  Emmerson Mnangagwa , amesema  amekutana  na  viongozi  wa  kidini  ambao  wanataka mjadala  wa  kisiasa  kati  ya  upinzani  na  rais.