1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani waapa kutoshiriki katika uongozi Sierra Leone

1 Julai 2023

Chama kikuu cha upinzani Sierra Leone kimesema hakitashiriki katika ngazi yoyote ya uongozi nchini humo, kutoka bunge hadi mabaraza ya miji.

https://p.dw.com/p/4TIxU
Sierra Leone | Präsidentschafts- und Parlamentswahlen | Samura Kamara
Picha: John Wessels/AFP/Getty Images

Chama cha All Peoples Congress - APC kimesema kinakataa matokeo yaliyotangazwa, ikizingatiwa dosari na ukiukaji wa taratibu zilizowekwa za uchaguzi.

Kimetoa msururu wa masharti, ikiwemo kujiuzulu kwa makamishena wa uchaguzi, kikiwatuhumu kwa upendeleo na kushindwa kufanya majukumu yao pasina kuegemea upande wowote.

Soma pia: Rais wa Sierra Leone aongoza matokeo ya uchaguzi

Aidha kimetaka uchaguzi uandaliwe upya katika miezi sita, kikisema zoezi hilo lazima lisimamiwe na watu wenye uadilifu na taasisi zitakazohakikisha mchakato wa haki na wazi.

Rais Julius Maada Bio alichaguliwa tena kwa muhula wa pili katika duru ya kwanza ya upigaji kura akiwa na asilimia 56.17 ya kura. Chama cha APC kikiongozwa na kiongozi wake Samura Kamara kilikuwa cha pili na asilimia 41.16 ya kura.