1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Uturuki wafungua kesi kupinga ushindi wa Erdogan

17 Mei 2023

Chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki kimesema leo kimewasilisha malalamiko kuhusiana na kile inachoshuku kwamba ni wizi wa kura katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita nchini humo.

https://p.dw.com/p/4RUeI
Bildkombo Recep Tayyip Erdogan und Kemal Kilicdaroglu
Picha: Burak Kara/Getty Images

Naibu mwenyekiti wa chama cha Republican People's Party (CHP), Muharrem Erkek, amesema kulikuwa na ukiukaji wa utaratibu wa upigaji kura katika maelfu ya masanduku ambapo katika baadhi ya masanduku kura zilihesabiwa vibaya.

Erkek amesema chama hicho awali kilikuwa kimepinga hesabu ya masanduku zaidi ya elfu mbili ya kura za urais na mengine karibu elfu tano ya kura za ubunge kote nchini humo.

Baada ya kupata chini ya asilimia 50 ya kura, Rais Erdogan atakuwa anaingia kwenye raundi ya pili ya uchaguzi ambapo atapambana na mpinzani wake mkuu Kemal Kilicdaroglu mnamo Mei 28.