1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Senegal umetangaza kuandamana leo

13 Februari 2024

Mashirika ya kiraia ya Senegal leo hii yamepanga maandamano kuendeleza shinikizo kwa Rais Macky Sall ambae amesogeza mbele terehe yauchaguzi wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4cKm6
Maandamano ya Senegal katika mitaa ya Dakar
Mwandamanaji wa Senegal akionyesha ishara wengine wakipiga picha wakati wa makabiliano na polisi wa kutuliza ghasia walipokuwa wakiandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais wa Februari 25, Dakar, Senegali Februari 9, 2024.Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Mashirika ya kiraia ya Senegal na upinzani waliendeleza shinikizo kwa Rais Macky Sall siku ya Jumatatu, ikiwa kabla ya maandamano yaliyopangwa kuendelea leo kwa lengo la kupinga kucheleweshwa kwa uchaguzi wa rais wa mwezi huu ambao tayari umezua machafuko mabaya kote nchini humo. Wanaharakati kutoka katika juhudi walioipa jina la "Tulinde uchaguzi wetu", ambayo inaundwa na makundi 40 ya kiraia, kidini na kitaaluma, wametoa wito wa maandamano mapya katika mji mkuu wa Dakar mchana wa leo. Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja miongoni mwa waratibu wa maandamano hayo, Abdou Khafor Kandji ametoa wito kwa raia wa Senegal kushiriki kwa amani katika maandamano ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi na kuongezwa kwa muda wa uongozi wa Rais Macky Sall. Uamuzi wa Sall wa kusogeza mbele uchaguzi wa Februari 25 umeitumbukiza Senegalkatika moja ya migogoro mibaya zaidi tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, huku maandamano ya ghasia yakisababisha vifo vya watu watatu.