1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upigaji kura waanza katika uchaguzi wa rais wa Mauritania

29 Juni 2024

Raia wa Mauritania leo hii wameanza kupiga kura kuamua iwapo watamchagua tena Rais Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani kama mkuu wa taifa hilo kubwa la jangwa.

https://p.dw.com/p/4hf2l
Mauritania | Uchaguzi wa Rais
Maafisa wa Uchaguzi wa Mauretania wakiangalia kadi za wapiga kura katika kituo cha kupigia kura huko Nouakchott Juni 28, 2024. Picha: JOHN WESSELS/AFP via Getty Images

Raia wa Mauritania leo hii wameanza kupiga kura kuamua iwapo watamchagua tena Rais Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani kama mkuu wa taifa hilo kubwa la jangwa, linalotazamwa kama chemchemi ya utulivu katika eneo lenye hali tete la Sahel.

Takriban wapiga kura milioni 1.9 waliojiandikishawanatazamiwa kuchagua kati ya wagombea saba wanaowania kuliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo kwa kiasi kikubwa limehimili wimbi la itikadi kali katika eneo hilo na linatazamiwa kuwa mzalishaji wa gesi.