1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thomas Müller kuongezewa mkataba Bayern Munich

8 Oktoba 2023

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Soka ya Ujerumani Bayern Munich, Jan-Christian Dreesen, amesema klabu hiyo imepanga kumuongezea muda mshambuliaji wake, Thomas Müller, kupindukia kipindi cha msimu huu.

https://p.dw.com/p/4XGXa
Fußball | Freundschaftsspiel Deutschland - Frankreich | Thomas Müller
Picha: Rolf Vennenbernd/dpa/picture alliance

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambao unafanana na ule wa mlinda mlango aliyejeruhiwa Manuel Neuer unamalizika mwisho wa msimu huu kisoka.Akizungumza na televisheni ya hapa Ujerumani ya Bild, Dreesen amesema wana sababu nzuri za kuendelea na Thomas kwa muda mrefu lakini pia alisema golikipa Neuer ataanza tena kucheza baada ya hali yake kuwa njema kulikotokana na kuvunjika mguu.