1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Union Berlin kushiriki Ligi ya Mabingwa?

24 Aprili 2023

Sheraldo Becker aliifungia Union Berlin pale klabu hiyo ilipopata ushindi wa 1-0 dhidi ya Borussia Mönchengladbach Jumapili.

https://p.dw.com/p/4QUEa
Borussia Mönchengladbach - 1. FC Union Berlin
Picha: Revierfoto/IMAGO

Ushindi huo katika mchuano wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga umezidisha matumaini ya Union kujikatia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwengineko Bayer Leverkusen Jumapili, waliwalaza mahasimu wao RB Leipzig 2-0 kwa magoli ya Adam Hlozek na  Nadiem Amiri aliyefunga mkwaju wa penalti. Kushindwa huko kumewapelekea RB Leipzig kutupwa nje ya timu nne bora kwa sasa.

1. Fussball Bundesliga; Bayer 04 Leverkusen - RB Leipzig
Adam Hlozek akipambana na Willi Orban wa LeipzigPicha: Teresa Kroeger/Nordphoto/IMAGO

Bayer Leverkusen kwa sasa wamekwenda mechi 13 bila kufungwa katika mashindano yote, wakati ambapo wanafukuzia nafasi ya kushiriki Champions League. Leverkusen pia wamefuzu kwenye nusu fainali ya Europa League.