1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto milioni 67 walikosa chanjo kwa sababu ya UVIKO-19

20 Aprili 2023

Umoja wa Mataifa umesema watoto milioni 67 walikosa baadhi ya chanjo au walikosa kabisa chanjo za kawaida kati ya mwaka wa 2019 na 2021 kwa sababu ya changamoto za huduma za afya zilizosababishwa na janga la UVIKO-19.

https://p.dw.com/p/4QLcm
Corona Virus Booster Impfung Konzept
Picha: Firn/Zoonar/picture alliance

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia watoto - UNICEF imesema mafanikio yaliyopatikana kwa taabu katika zaidi ya muongo mmoja katika utoaji chanjo za kawaida kwa watoto yameondolewa.

UNICEF imeelezea wasiwasi wa kuzuka miripuko ya ugonjwa wa kupooza - polio na surua. Utoaji chanjo kwa watoto ulipungua katika nchi 112 na asilimia ya watoto waliopewa chanjo kote ulimwenguni ilishuka kwa pointi tano hadi asilimia 81, ikiwa ni idadi ya chini mno ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka wa 2008. Afrika na Kusini mwa Asia ndio maeneo yaliyoathirika zaidi.