1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yataka sheria ya usalama Hong Kong ibadilishwe

Ibrahim Swaibu
4 Septemba 2020

Umoja wa Mataifa umeitisha uchunguzi huru na wa kina kuhusu sheria ya Usalama ambayo China ilianzisha Hong Kong.

https://p.dw.com/p/3i1JX
Deutschland  Demonstration für Hongkong in Berlin
Picha: Getty Images/AFP/T. Schwarz

Katika barua iliyotolewa leo Ijumaa, wajumbe maalum wa umoja huo wamesema sheria hiyo yenye utata inatishia haki za kimsingi na kukandamiza uhuru wa kujieleza. 

Katika barua hiyo ambayo imetolewa kwa wandishi habari na yenye kubeba ujumbe kwa serikali mjini Beijing, wajumbe maalum wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wamesema sheria ya Usalama ya China katika kisiwa cha Hong Kong inatishia haki za kimsingi za binadamu huku wakionya kuwa huenda itatumiwa kuwashtaki wanaharakati wa kisiasa.

Aidha imeeleza kuwa mbali na kukandamiza uhuru wa kujieleza sheria hiyo pia inawanyima majaji na mawakili wa Hong Kong fursa ya kutenda kazi yao kwa huru.

"Sheria ya Usalama wa taifa inatishia uhuru wa kimsingi na inaweza kukiuka harakati za kulinda uhuru huo” imeeleza sehemu ya barua hiyo na kuonya kuwa sheria hiyo itakandamiza uhuru wa watu kutoa maoni yao, uhuru wa kujieleza pamoja na haki ya kufanya mikutano ya amani.
 

Umoja wa Mataifa umetaka kufanyika kwa uchunguzi huru na wa kina kuhusu sheria hiyo ili kuhakikisha kwamba inaenda sambamba na jukumu la China la kulinda haki za binadamu. Hata hivyo kwa upande wake China imewataka wajumbe hao kuacha kuingilia katika masuala ya ndani ya nchi hiyo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema

Mamlaka katika mji wa Beijing pamoja na zile za Hong Kong zinasema sheria hiyo inahitajika ili kuhakikisha utulivu na ustawi wa kisiwa hicho.
Mamlaka katika mji wa Beijing pamoja na zile za Hong Kong zinasema sheria hiyo inahitajika ili kuhakikisha utulivu na ustawi wa kisiwa hicho.Picha: picture-alliance/Kyodo

"Sheria ya Usalama wa taifa katika mji wa Hong Kong sio suala la haki za binadamu. Lengo la sheria hiyo ni kuziba mapungufu ya awali katika suala la Usalama wa taifa Hong Kong, na kuzuia vitendo vya aina yote yote vinaohatarisha Usalama wa taifa.Sheria hiyo inawaadhibu wachache na kuwalinda walio wengi. Haina athari yoyote kwa haki na uhuru halali wa wakaazi wa Hong Kong. Na kwa hivyo, wakaazi wengi wameiiunga mkono sheria hiyo,” amesema Hua Chunying.

Barua hiyo yenye kurasa 16 ilitumwa na Fionnuala Ni Aolain, mjumbe maalum wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa akiwa pamoja na wajumbe wengine 6.

Kulingana na wajumbe hao, sheria hiyo ambayo inataja makosa ya uchochezi, ugaidi, kujitenga na kupanga njama au kushirikiana na mataifa ya kigeni kama makosa yanaoyohatarisha usalama wa taifa, imesababisha idadi kubwa ya waandamanaji na wanaharakati nchini Hong Kong kubaki kimya.

Mamlaka katika mji wa Beijing pamoja na zile za Hong Kong zinasema sheria hiyo inahitajika ili kuhakikisha utulivu na ustawi wa kisiwa hicho.

Lakini wajumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wanasema sheria hiyo haipaswi kutumiwa ili kuzuia, au kukandamiza uhuru wa kimsingi ambao unalindwa kisheria kama vile uhuru wa mtu kutoa maoni, uhuru wa kujieleza pamoja na ule wa kufanya mikutano.

Aidha wajumbe hao wana khofu kuwa huenda sheria hiyo itatumiwa kupiga marufuku harakati zote za watatetezi wa haki za binadamu katika kisiwa hicho licha ya harakati hizo kufanyika kwa njia halali za kisheria.

Hata hivyo kwa upande wake, China kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje Hua Chunying imewataka wajumbe hao kuachia kuangilia kati katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.