1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN yataka mzingiro wa kijeshi wa El-Fasher Darfur ukomeshwe

14 Juni 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotaka kukomeshwa kwa mzingiro wa kijeshi kwenye mji wa Sudan wa El-Fasher.

https://p.dw.com/p/4h1rW
Azimio hilo lililoandaliwa na Uingereza lilipitishwa na nchi wanachama 14 miongoni mwa jumla ya 15, huku Urusi ikijizuia kupiga kura.
Azimio hilo lililoandaliwa na Uingereza lilipitishwa na nchi wanachama 14 miongoni mwa jumla ya 15, huku Urusi ikijizuia kupiga kura.Picha: Michael M. Santiago/Getty Images

El-Fasher ndio mji mkuu pekee wa jimbo la Darfur lililoko magharibi mwa nchi hiyo na ambako zaidi ya watu milioni moja wanaripotiwa kuzingirwa. 

Azimio hilo limetaka kikosi cha wanamgambo wa RSF pamoja na jeshi la Sudan kusitisha mara moja uhasama na kuwezesha kumalizika kwa vita hivyo ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Limeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu machafuko yanayozidi kutanuka na ripoti za kuaminika kwamba wanamgambo wa RSF wanaendeleza kile lililolitaja kuwa machafuko ya kikabila katika mji mkuu wa Darfur Kaskazini- El, Fasher. Mwaka uliopita, machafuko kama hayo pia yalifanyika katika mji wa El Geneina, magharibi mwa Darfur.

Barbara Woodward: Shambulizi la El-Fasher laweza kuwa na maafa mabaya

Baada ya kura hiyo, balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Barbara Woodward, aliliambia baraza la usalama la umoja huo kwamba "Kupitishwa kwa azimio hili kunatuma ujumbe wa wazi kwamba ni sharti wanamgambo wa RSFwaache mara moja mzingiro wao wa El Fasher na kwamba pande zote lazima zisitishe mapigano. Shambulizi dhidi ya mji huo unawza kuwa na maafa mabaya kwa wakaazi wake milioni 1.5."

Ukatili dhidi ya watoto katika migogoro ulifikia viwango vya juu zaidi 2023

Vurugu zauwa watu 38 El-Fashir Sudan

Mji huo ndio pekee salama unaowahifadhi watu waliokimbia machafuko na mashirika ya misaada yameonya kuhusu hali mbaya ya kiutu kutokana na mapambano yanayoendelea.

Hujuma za RSF zasababisha kufungwa hospitali muhimu Sudan

Sudan ilitumbukia kwenye machafuko mnamo Aprili mwaka 2023, wakati mvutano kati ya wakuu wa pande mbili za kijeshi uligeuka kuwa vita katika mji mkuu Khartoum na kisha kuenea hadi maeneo mengine ikiwemo Darfur.

Umoja wa Mataifa unasema hadi sasa, zaidi ya watu 14, 000 wameuawa na 33,000 wamejeruhiwa.

Hofu ya kurudi kwa mauaji ya kimbari Darfur

Miongo miwili iliyopita, Darfur ilihusishwa mara kwa mara na mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita, uliofanywa hasa na wanamgambo wa kiarabu Janjaweed.

Mwaka mmoja wa vita vya Sudan

Takriban watu 300,000 waliuawa na milioni 2.7 walilazimika kuyakimbia makwao.

Mizozo iliopo kwenye mataifa ya Afrika imesahaulika?

Kuna hofu kwamba huenda jinamizi hilo limerudi. Mnamo Januari, mkuu wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya Jinai Karim Khan alisema zipo sababu za msingi kuamini kwamba pande mbili husika katika machafuko ya sasa ya Sudan zimefanya uhalifu wa kivita, dhidi ya ubinadamu au zimefanya mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.

(APE, EBU)