1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiLibya

UN yasema wahamiaji wameteswa na kufanywa watumwa Libya

27 Machi 2023

Uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa umebaini kuwa wahamiaji waliokwama nchini Libya walipokuwa wakijaribu kuingia barani Ulaya wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

https://p.dw.com/p/4PJlP
Ocean Viking I Migranten aus dem Mittelmeer gerettet
Picha: Vincenzo Circosta/AA/picture alliance

Vitendo hivyo vinajumuisha mateso na kulazimishwa kuwa watumwa wa ngono.

Aidha ripoti ya uchunguzi huo imebaini kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na kwamba inaaminika kuwa idadi kubwa ya uhalifu huo umefanywa na vikosi vya usalama vya serikali na vikundi vya wanamgambo wenye silaha.

Hata hivyoy, jopo la watu waliofanya uchunguzi huo limesema karibu manusura wote waliowahoji hawakushtaki kwenye vyombo husika kwa kuwa hawana imani katika mfumo sheria na pia walihofia kukamatwa, kuteswa au kunyang'anywa mali zao.

Libya imekuwa katika mzozo kwa zaidi ya muongo mmoja tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu, Muammar Qaddafi.