1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yapitisha azimio la vikwazo kwa Gaddafi

27 Februari 2011

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio la kumuwekea vikwazo kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/10Q94
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano New YorkPicha: AP

Azimio hilo linajumuisha kuzuia mali, marufuku ya kusafiri kwa Gaddafi na baadhi ya wanafamilia yake pamoja na kutekeleza vikwazo vya silaha.

Baraza hilo la usalama pia limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya The Hague, kuchunguza ukandamizaji uliofanywa dhidi ya raia wa Libya, uamuzi ambao umepokelewa na balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa, Peter Wittig.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa nchini Libya katika kipindi cha siku kumi zilizopita kutokana na ghasia.

Mwandishi:Grace Patricia Kabogo (RTRE,AFP,DPA)
Mhariri:Maryam Dodo Abdalla