1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya, raia wa Tigray wanakabiliwa na kitisho cha njaa

26 Mei 2021

Afisa mmoja mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amelionya Baraza la Usalama kuwa hatua za dharura zinahitajika ili kuepusha baa la njaa katika mkoa ulioharibiwa kwa vita wa Tigray nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/3tynZ
Äthiopien I Konfliktregion Tigray
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mkuu wa masuala ya kiutu na Mratibu wa msaada wa dharura Mark Lowcock amesema kuna kitisho kikubwa cha baa la njaa kama msaada hautaimarishwa katika miezi miwili ijayo.

Amesema asilimia 20 ya idadi ya watu wa Tigray wanakabiliwa na uhaba wa dharura wa chakula, na kuwa uharibifu na mashambulizi dhidi ya raia yanaendelea mpaka sasa katika eneo hilo.

soma zaidi: Marekani yaiwekea vikwazo Ethiopia na Eritrea

Ikiwa ni zaidi ya miezi sita baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AHmed kuanzisha kile alichoita operesheni ya kasi ya kijeshi, mapigano na ukiukaji wa haki vimeendelea Tigray, ambako kitisho cha njaa kimekuwa kikilikabili kwa miezi kadhaa.