1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN. yaonya dhidi ya ukandamizaji wa wanawake Afghanistan

9 Machi 2023

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan ameonya kwamba ukandamizaji wa haki za wanawake unaofanywa na utawala wa Taliban huenda ukapelekea kupunguzwa kwa fedha za misaada na maendeleo kwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4OQdQ
Indien | Afghanische Schülerinnen im indischen Exil
Picha: Adil Bhat/Sharique Ahmad/DW

Roza Otunbayeva ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, marufuku ya utawala wa Taliban kwa wanawake kujiunga na shule za sekondari na vyuo vikuu, kutembelea mabustani na kufanya kazi katika mashirika ya misaada, ni mambo yanayoweka hatari misaada kwa nchi hiyo.

Wanawake nchini humo pia hawakubaliwi kutoka nje bila kuandamana na jamaa yake ambaye ni mwanamume.

Otunbayeva amesema mazungumzo kuhusiana na kuisaidia nchi hiyo katika miradi ya maendeleo yamesitishwa kutokana na marufuku hayo ya wanawake Afghanistan.