1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yakaribisha hatua ya kusitisha mapigano kwa muda Gaza

16 Juni 2024

Umoja wa Mataifa umekaribisha uamuzi wa Israel wa kusitisha mapigano Kusini Mwa Gaza kwa masaa kadhaa kila siku, ili kuruhusu misaada ya kibinaadamu kufikishwa kwa Wapalestina wanaokumbwa na vita.

https://p.dw.com/p/4h6ii
Israel
UN yakaribisha tangazo la Israel la kusitisha mapigano kwa muda Gaza kuruhusu misaada zaidi kupelekwa katika eneo hiloPicha: Amir Levy/Getty Images

Umoja huo lakini kupitia msemaji wa shirika lake la kuratibu misaada ya dharura OCHA Jens Laerke limetoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kutozuwia misaada zaidi kuingizwa katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa wa msaada huo wa kibinaadamu. 

Israel kusitisha mapigano kwa muda kila siku Gaza

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na makundi ya misaada ya kiutu yamekuwa yakitahadharisha kuhusu ukosefu wa chakula na mahitaji mengine muhimu katika Ukanda wa Gaza yaliyosababishwa na kuzuwiwa kwa misaada hiyo na kufungwa kwa njia ya kupitishia misaada hiyo ya Rafah inayopakana na Misri tangu Israel walipodhibiti eneo hilo mwanzoni mwa mwezi Mei. 

Jeshi la Israel lilitangaza kusitisha mapigano hayo kila siku katika eneo hilo la Kusini mwa Rafah kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni. Hatua hiyo itafanyika kila siku hadi taarifa nyengine itakapotolewa.