1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wanajeshi 3,000-4,000 wa Rwanda walipelekwa Kongo

11 Julai 2024

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kati ya wanajeshi 3,000 na 4,000 wa Rwanda walipelekwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kushirikiana na waasi wa M23.

https://p.dw.com/p/4i8AR
Kibumba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 2022 | Waasi wa M23
Waasi wa kundi la M23 wakiwa kwenye moja ya harakati zao katika kijiji cha Ikumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Disemba 23, 2022Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Wataalamu hao wamesema wanajeshi hao wa Rwanda walipelekwa kwenye mikoa iliyoko mashariki mwa jimbo la kivu Kaskazini ya Nyiragongo, Rutshuru na Masisi, walipokuwa wakiandaa ripoti yao mwezi Aprili.

Wataalamu hao walisema uingiliaji wa jeshi la Rwanda na operesheni zake kwenye maeneo hayo matatu, yalikuwa ni muhimu katika harakati za kujitanua zilizofanikiwa kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu.

Jopo hilo aidha limesema mzozo wa M23 unaoongezeka unaibua kitisho cha kuzua mgogoro mkubwa zaidi wa kikanda.