1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN na AU zahimiza amani kufuatia machafuko Senegal

3 Juni 2023

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika umetoa wito wa amani nchini Senegal baada ya kutokea machafuko na kusababisha serikali kupeleka wanajeshi mitaani ili kudhibiti hali.

https://p.dw.com/p/4S9d0
Senegal Unruhen nach Urteil gegen Sonko
Picha: Guy Peterson/AFP

Watu 9 waliuwawa siku ya Alhamisi baada ya kiongozi maarufu wa upinzani Ousmane Sonko kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili, kwa kosa la kuwachochea vijana, na huenda hilo likamuondoa katika azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2024. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilaani machafuko hayo na kuomba pande husika kuvumiliana na kuepuka vurugu. 

Rais wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amewataka viongozi hao kuchukua hatua na kulinda demokrasia ya Senegal ambayo Afrika imekuwa ikijivunia. Nayo Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, imetoa wito kwa pande zote kulinda hadhi ya taifa hilo ya amani na udhabiti.