1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mfumo wa hifadhi ya wakimbizi wa Rwanda haujitoshelezi

11 Juni 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa lenye kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema mfumo wa uhifadhi wa wakimbizi wa Rwanda bado haujitoshelezi.

https://p.dw.com/p/4gt5v
Uingereza | Tukio la ukumbusho la maadhimisho ya miaka 80 ya D-Day huko Portsmouth, Uingereza
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akizungumza wakati wa hafla ya ukumbusho wa kumbukumbu ya miaka 80 ya D-Day, huko Portsmouth, Uingereza, Juni 5, 2024. Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Shirika hilo limesema limepata ridhaa ya kuichagiza Mahakama Kuu ya Uingereza, kutokana na sera ya taifa hilo yenye kutaka kuwapeleka wanaotafuta hifadhi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Wanasheria wanaomuwakilisha Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi wanasema kuwapeleka wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda kunawaweka katika hatari ya kuhamishiwa katika nchi nyingine ambako wanaweza kukabiliwa na aidha kifo au mateso. Awali akijibu wasiwasi huo wa kiusalama, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema Rwanda lazima itazamwe kama taifa salama.