1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mashambulizi Gaza huenda ni uhalifu wa kivita

27 Mei 2021

Mkuu wa baraza la UN kuhusu haki za binadamu Michelle Bachellet amesema mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza huenda yakachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita

https://p.dw.com/p/3u2tS
Palästina | Zerstörtes Gebäude in Gaza
Picha: Suhaib Salem/REUTERS

 

Akifungua kikao maalum cha baraza hilo la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kilichoandaliwa kufuatia ombi la mataifa ya Kiislamu, Bachellet (Soma Bashelee)  amesema kuwa iwapo mashambulio hayo ya Israel yatathibitishwa kuwa ya kiholela na yasiofaa na kuwaathiri raia na mali ya raia, yatachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita.

Bachellet ameongeza kuwa licha ya madai ya Israel kwamba majengo hayo yalikuwa makazi ya wapiganaji wa kujihami ama kutumika kwa shughuli za kijeshi, bado hakujapatikana ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

Wito katika pendekezo

Pendekezo lililo mbele ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu linatoa wito wa uchunguzi wa hali ya juu kuhusu dhuluma na vyanzo vyake katika mzozo wa miongo kadhaa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Michelle Bachelet | UN Hochkommissarin für Menschenrechte
Michelle Bachelet- Mkuu wa baraza la haki za binadamu la UNPicha: picture-alliance/Keystone/S. Di Nolfi

Rasimu hiyo ya maazimio ilyowasilishwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC itajadiliwa wakati wa kikao hicho maalum cha siku moja kinacholenga kuzungumzia ongezeko la vurugu mbaya kati ya Waisraeli na Wapalestina mwezi huu.

Watakao hutubia kikao

Waziri wa mambo ya nje wa Mamlaka ya Palestina Riyad-al- Maliki ni miongoni mwa wale wanaotarajiwa kuhutubia kikao hicho pamoja na Meirav Elion Shahar ambaye ni balozi wa Israeli katika Umoja wa Mataifa nchini Uswisi.

Rasimu hiyo inayotarajiwa kupigiwa kura baadaye leo, inatoa wito kwa baraza hilo kuanzisha kwa haraka tume huru ya uchunguzi ya kimataifa katika eneo hilo la Palestina lililokaliwa pamoja na Yerusalemu ya Mashariki na Israeli.

Blinken akamilisha ziara yake ya Mashariki ya Kati

Wakati huo huo, katika kituo cha mwisho cha Blinken katika ziara yake ya Mashariki ya Kati, alikutana na mfalme wa Jordan Abdullah 11 mjini Amman ambapo baadaye aliwahutubia wanahabari na kusema kuwa kupatikana kwa makubalino hayo ya kusitisha mapigano kulikuwa muhimu hasa kutokana na athari zilizokumba familia za pande zote mbili na kwamba hawachukulii makubaliono hayo kuwa mwisho bali mwanzo wa suala muhimu linaloweza kufuatiliwa.